Nyanya ni zao la mboga mboga ambalo ulimwa kwa ajili ya kibiashara na chakula . Kitaalamu ujulikana Kama Solanum lycopersicum kutoka familia ya Solanaceae.
Nyanya hulimwa majira yote ya masika na kiangazi
-Nyanya Kama Eden F1 , Peseo F1, Ghama F1, Perseo F1, hulimwa wakati wa masika.
-Nyanya Kama Assila F1, Jarrah F1, Imara F1, Perseo F1, hizi ulimwa wakati wa kiangazi.
Tunda hili hustawi vizuri kwenye mazingira yenye joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-30oC .
UDONGO
Aina za udongo kuanzia kichanga , tifutifu, ili mradi uwe na rutuba na husiotuamisha maji. Udongo wenye tindikali Kati ya 6.0 -7.0ph ndo hufaa kwa kilimo Cha dawa
Joto chini ya sentigredi 18 hufanya mmea kutoa matawi mengi na kuzaa matunda madogomadogo . Hali ya mvua nyingi na baridi Kali husababisha kuenea kwa magonjwa na wadudu waharibifu . Hivyo mkulima akipanga kulima masika jianda kupambana na magonjwa ya mlipuko .
AINA ZA NYANYA
Kuna aina mbili za nyanya ambazo ni ;-
- Nyanya fupi (Detarminant)
Mfano ;- Imara F1, Rio grand , Eden F1, Jarrah F1, Tanya , Red cloud , Roma VF. - Aina ya nyanya ndefu ( Intermediate)
Mfano;- Anna f1, Mandel , Eva f1, Tengeru 97, Tylka f1.
AINA ZA MBEGU ZA NYANYA
Mbegu za nyanya zimegawanyika katika makundi 2 - Mbegu zilizoboreshwa ( Open pollinated variety -OPV)
Mfano wa nyanya hizi za kawaida zilizoboreshwa ni Kama;- Tengeru , Tanya, Mwangaza, Mkulima nk - Mbegu chotara ( Hybreed)
Mfano wa mbegu chotara ni Eden F1, Assila F1, Ghama F1, Imara F1, Kipato f1, Perseo F1, Anna F1, nk
Wakulima wanashauliwa kulima nyanya aina ya chotara kwa Mazao Bora na mengi pia hizi mbegu hukomaa mapema, nyanya zenye matunda mengi zenye ganda gumu ili yawe rahisi kusafirishwa , inahimili maradhi ya mwanzo aina ya Alternalia stem cancer, mnyauko aina ya fusarium wilt, minyoo fundo ( nematodes) , mavuno yake kuanzia tani 25 kwa hekari endapo shamba litahudumiwa vizuri.
KITARU CHA KUOTESHA MBEGU ( Nursery)
Kitalu; hii ni sehemu ambapo Miche huoteshwa na kutunzwa kabla ya kupelekwa kupandikizwa shambani.
UTAYALISHAJI
Ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo wakati wa kuchagua sehemu ya kitalu
- Eneo la kitaru lisiwe na magugu sugu Kama ndago
- Eneo liwe na udongo wenye rutuba
-Kitalu kisiwe mbali Sana na bustani - Eneo liwe karibu na maji ya kutosha kwa ajili ya umwagiliaji
- Eneo liwe tambarare
- Eneo liwe na miti kandokando ya kukinga upepo
- Eneo liwe na mwanga wa jua wa kutosha AINA ZA VITARU
- Kitalu Cha sahani ( Trays)
- Kitalu Cha ardhini KUOTESHA MBEGU KWENYE TRAY
Hii ni njia nzuri Sana kuotesha mbegu za nyanya hasa za chotara ( Hybreed) kutokana na ughali wa mbegu hizi , mbegu zilizooteshwa kwenye trei husaidia kuepuka magonjwa ya ardhini na Miche hukua vuzuri na kwa haraka zaidi .
KITALU CHA ARDHINI
Andaa Eneo la kuweka Kama Kuna nyasi, visiki, au uoto wowote huondoe kwa kufyeka na kukusanya pamoja , katua udongo na kuulainisha kwa kutumia jembe , weka samadi kwenye kitalu debe moja kwa tuta la upana na urefu wa mita1 Kisha changanya na udongo halafu sawazisha na reki , mbolea au mboji iwekwe siku 3 na kumwagiliwa maji.
JINSI YA KUPANDA MBEGU
Kuna aina kuu mbili za kupanda mbegu kwenye kitalu Kama ifuatavyo;-
- Kupanda kwa kutawanya
- Kupanda kwa msitari;- Unatakiwa kutengeneza mifereji (Drills) ,pima sentimeta 10 kutoka msitari na msitari , sia mbegu katika msitari uliotengenezwa Kisha fukia kwa udongo kidogo .
NB;- Kabla hujasia mbegu changanya na mchanga kwa kipimo Cha kijiko kimoja cha mbegu kwa vijiko 3 vya mchanga (1:3:4) au kikombe kimoja Cha mbegu kwa vikombe 3 vya mchanga.
Baada ya kupanda mbegu mwagilia asubuhi au jioni kila siku, funika kitalu chako kwa matandazo ,baada ya mbegu kuota funua matandazo
Mbegu huwa tayari kuamishiwa shambani baada ya wiki 3-4 KUAMISHA MICHE TOKA KITAKUNI KWENDA SHAMBA ( Main field )
- Mmea unavyofikisha wiki 3-4 na kuwa na majani zaidi ya 3 huwa tayari kuamishiwa shambani ( main field)
-Mwagilia Miche masaa machache kabla ya kuhamishia shambani ili wakati wa kungoa miche , mizizi ishikamane vizuri na udongo
-Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, Miche yote iliyonyongonyea na myembamba kupita kiasi hisichukuliwe wakati wa kupeleka shambani .
-Ngoa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi hisidhurike.
JINSI YA KUANDAA SHAMBA
- Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1 kabla ya kupanda Miche, ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa
- Wakati wa masika au mvua nyingi inashauliwa kupanda nyanya kwenye matuta ili zisiathiliwe na maji na wakati wa kiangazi unaweza kupanda nyanya pasipo kutengeneza matuta. Lakini ni muhimu kupanda nyanya kwenye matuta
- Wakati wa kipindi Cha baridi ni vema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzunguko wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi
NAFASI YA UPANDAJI
Nyanya hupandwa Kati ya sentimita 50-75 mche na mche na Kati ya 70 hadi 90 msitari na msitari.
Nyanya huweza kupandwa shambani kwa mstari mmoja mmoja katika tuta na mistari miwili (Double Row) katika tuta.
MATUNZO YA SHAMBA
Baada ya kupandikiza nyanya shambani , shamba la nyanya linatakiwa kutunzwa ili uweze kupata mavuno mengi na bora , mambo yanayofanyika ni Kama ifuatavyo;-
- Matandazo;- Matandazo ni mabaki ya mimea na nyasi kavu ambazo hutumika kufunika ardhi kwa lengo la kuhifadhi unyevunyevu, kudhibiti magugu , kupunguza mmomonyoko wa udongo, kuongeza rutuba pale yanapooza, pia Kuna matandazo ya plastik ( plastic mulches)
- Umwagiliaji;- Nyanya huitaji maji mengi Sana kwa ajili ya ukuaji wa mimea na matunda yake. Hutakiwi kubadirishs kiasi Cha maji Wala ratiba ya kumwagilia maji, maji yakizidi Sana kwenye shamba la nyanya huweza kuleta tatizo kwenye tunda la nyanya vile vile yakipungua Sana huleta tatizo , upungufu wa maji usababisha kudondosha au kupukutisha maua ( Blossom drop)
- Kusimika miti;- Nyanya zinatakiwa ziwekewe miti au mambo ili kuzuia zisianguke au kutambaa kwenye udongo Jambo ambalo linaweza kusababisha madhara mengi kwenye nyanya ikiwemo wadudu ,magonjwa na nyanya kuchomwa na joto Kali la ardhini , kusimika miti hufanywa wiki ya 2 baada ya kupandikiza
- Kufunga nyanya kwenye miti;- Aina ndefu ya nyanya ni lazima ifungwe kwenye miti ili kuzuia mmea husitambae chini . Mimea iliyofungwa kwenye miti huraisisha unyunyiziaji wa dawa, umwagiliaji na uchumaji wa matunda
- Kupunguza matawi;- Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa hewa na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya majani yanayoondolewa ni Yale yaliyoonyesha dalili za magonjwa , kushambuliwa na wadudu na yaliyozeeka , pia usaidia kupunguza maambukizi ya ukungu katika shina, majani yapunguzwe kipindi Cha asubuh kwa kutumia mkono na sio kisu kwani kinaweza kueneza magonjwa
- Kukata kilele Cha nyanya;- Kwa kawaida aina ndefu ya nyanya huzaa ngazi zaidi ya sita za matunda lakini mmea una uwezo wa kubeba ngazi 5-6 tu za matunda, kata kilele mimea inapokua na ngazi 5 na Jani moja liache juu ya ngazi ya mwisho ( 6) , ni muhimu kukata sehemu ya juu ya mmea ili kuimarisha ukuaji wake. Machipukizi yote yanayojitokeza pembeni inabidi yaondolewe ili kupata matunda makubwa na yatakayoiva haraka.
UWEKAJI WA MBOLEA
Nyanya huitaji virutubisho ambavyo ni muhimu katika ukuaji wa mmea , Virutubisho hivyo huongeza rutuba na uzalishaji kwenye udongo .
MBOLEA ZA KUPANDIA
Baada ya kuandaa matuta au shamba lako , tengeneza mashimo ya nyanya na uweke mbolea ya samadi au mboji mikono miwili unaeza kuchanganya na mbolea ya kuku mkono mmoja siku 3 kabla ya kupanda ili samadi iweze kuoza vizuri , ichanganywe na udongo na kumwagia maji mpaka utakapopanda Miche yako.
Mbolea za kupandia za viwandani ni zile mbolea ambazo Zina kiwango kikubwa Cha Phosphorus P kwa ajili ya kusaidia uhotaji wa mizizi , mbolea hizi huwekwa shambani siku ya kupanda au siku moja kabla ya kupanda Miche yako . Mbolea hizo ni pamoja na Yaramila OTESHA , DAP, TSP, NPK yenye namba zinazolingana au yenye namba kubwa ya Kati (17:17:17) (10:20:10)
Weka gram 10 kwa kila shimo
MBOLEA YA KUKUZIA
Mbolea za kukuzia nyanya ni zile zenye Nitrogen kubwa , huwekwa shambani wiki ya 2-3 baada ya mmea kuota vizuri,
Mbolea hizo ni pamoja na SA yenye N 21%, CAN 26% N, UREA 46%N , YaraMila winner, na NPK yenye namba kubwa ya mwanzoni ( 25:5:5)
Mbolea hizi huwekwa kukiwa na hali ya unyevunyevu katika udongo, weka gram 10 kwa kila mmea , unaweza kutumia kizibo Cha soda kimoja na robo .
MBOLEA ZA KUZALISHIA
Hizi ni mbolea zenye kiwango kikubwa Cha Potassium K na huwekwa kwenye nyanya kipindi Cha maua na matunda kutokea kwenye nyanya
Mbolea hizi huwezesha matunda kukomaa na kuiva mapema, huwezesha kutengeneza mbegu bora , ongezeko la maji kwenye mmea
Mbolea hizi ni Kama MOP ( potassium chloride 48-60%K), NPK yenye K kubwa (5:5:20) , Yaramila winner na YaraLiva Nitrabor ( Ca+B) 15.4%N+25.9%CaO 0.3%B
MBOLEA ZA BOOSTER
Mbolea hizi ni zile zinazopigwa kwenye majani
1.Booster za kukuzuia ni Kama Agri grow, Booster ya NPK yenye namba zinazofanana ( 17:17:17) au zenye namba kubwa ya mwanzoni (20:10:10)
- Maua yanapotoka ni Kama Vigmax,Agri grow, Easy grow, Yara Vita trace BZ ( mg, b, na zn) ,Omex folia feltilizer nk
3.Booster wakati wa matunda (Finisher booster), hizi hutumika wakati wa matunda yanapoanza kutoka
Ni Kama MULT K classic, YaraVita Tracel BZ , Polyfeed finisher nk
NB: Wakati wa maua na matunda unaweza kuchanganya mbolea za YaraLiva Nitrabor + Yaramila winner hii itaendelea wakati wote wa matunda adi unapovuna
INAENDELEA…………
WADUDU SUMBUFU
- Funza wa vitumba ( Fruit worm)
Hushambulia nyanya wakiwa funza wachanga ,hula majani na baadae matunda
KUTHIBITI: Chunguza Mara kwa Mara ili kubaini funza Hawa Kama wapo- chuma na teketeza matunda yalioathikika
- fanya mzunguko wa Mazao
- Epuka kupanda nyanya karibu na pamba au mahindi
DAWa: Tumia dawa Kama vile Farmguard, Dudu Acelamectin , Duduba.
- Utitili mwekundu ( red spider mites)
Dalili: hujumuisha madoa ya manjano kwenye majani pamoja na hali Kama ya kuungua kwenye majani na matunda ikifuatiwa na utando Kama wa buibui
Mashambulizi yakizidi mmea husababisha umanjano wa majani na matunda , kupukutika kwa majani , kukauka kwa mti kuanzia kileleni na kufa kwa mmea
DAWA;
Tumia dawa Kama Abamectin, Ninja, Cutter, Karate , Duduall nk - Inzi weupe . Hawa ni wadudu wadogo Sana ambao hukaa chini ya majani ya nyanya hasa yale majani machanga ya juu, ufyonza maji maji kwenye majani
DAWA
Puliza sumu Kama vile Actara, Super Kinga, Cutter, Confidor nk
4.Minyoo fundo (Root knot nematodes)
Dalili; hujumuisha umanjano na kudumaa kwa mmea , kunyauka na hatimae kuoza , wadudu hawa hushambulia mizizi ya nyanya
KUDHIBITI;
Dumisha kiwango kikubwa Cha mbolea za asili ( samadi au mboji kwenye udongo
Ngoa na uchome Moto mimea iliyoathirika na takataka zote za mazao
Tumia kilimo Cha mzunguko
Tumia mbegu zenye uwezo wa kustahimili minyoo fundo Kama vile Tengeru , perseo f1, meru, Roma VFN - Chorachora (Leaf minner);
Ni funza wa wadudu mbalimbali ambao hufyonza maji ya majani ya nyanya
KUTHIBITI
Pulizia sumu Kama Cutter, Atacan, Duduba, Dudu Acelamectin nk MAGONJWA - Bakajan chelewa (late blight)
Ugonjwa huu huenezwa na vimelea vya fangasi , husababishwa na hali ya hewa hasa ya unyevu nyevu ,ukungu, pia uenezwa na upepo
Dalili; Huonekana kwenye Jani la chini , majani na shina huwa na mabaka makubwa yenye rangi nyeusi au kahawia nzito
DAWA; Ridomil gold, Dithane 45, Copper oxychloride nk
2.Bakajani tangulia (Early blight)
Huenezwa na vimelea vya fangasi , uenezwa na kusababishwa na Hali ya hewa Kama unyevunyevu , ukungu , upepo pamoja na mbegu zenye magonjwa
Dalili; huanza kuonekana kwenye kingo na pembezoni mwa majani , kingo za majani huwa na rangi nyeusi iliyochanganyika na kahawia yenye mabaka ya kahawia ya mviringo
UTHIBITI;
Tumia mbegu Safi na Bora
Teketeza mazao baada ya kuvuna
Nyunyizia sumu za Ridomil gold, Funguran, Snow power, Topsin M 70
3.Mnyauko fusari ( fusarium wilt)
Husambazwa na vimelea vya fangasi vinavyoishi kwenye udongo
UTHIBITI;
Tumia mbegu Safi na bora.
Tumia mzunguko wa Mazao
Choma kitaru Cha nyanya kabla ya kusia mbegu
Tumia sumu Kama vile Ridomil gold+innovex, Topsin M 70, Root shield ( Dawa hii iwekwe au kunyunyizia kwenye udongo)
4.Mnyauko bacteria( Bacteria wilt)
Usababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye udongo
Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafla hasa wakati wa jua Kali , baadae hudumaa majani na vikonyo vyake hukunjamana na kufa
UDHIBITI - Panda nyanya sehemu ambapo hapajawahi kupandwa viazi mviringo, bilinganya, hoho, au nyanya chungu
- Hakikisha mifereji ya kumwagilia hayapitii kwenye shamba lenye historia ya ugonjwa huu
- Kuepuka kuweka mbolea nyingi za samadi au chumvi chumvi
- Choma kitaru Cha nyanya kabla ya kusia
KIASI CHA MBEGU
Gram 25-35 kwa mbegu za chotara utosha hekali moja
Ambapo gramu moja ya mbegu Ina mbegu 300-320,
Hekali moja huitaji Kati ya miche 5800-9000 kutegemea na nafasi ya upandaji , Aina ya mbegu, udongo na sehemu.
Kwa mbegu za kawaida OPV ni gram 120-140 kwa hekali mojaIMEANDALIWA NA
CALVIN GASPER
Leave a comment